0
Luis Enrique wanted to reprimand Messi
 
Katika kile kinachoonekana kama ni hali ya mambo kutokuwa sawa ndani ya klabu ya Barcelona ijumaa iliyopita ilitokea hali ya sintofahau baina ya meneja wa klabu hiyo Luis Enrique na mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi.
 
Kwenye sintofahamu hiyo iliyotokea mazoezini nusura wawili hao watandikane makonde wakati wakiwa kwenye mazoezi ya kawaida ya klabu hiyo.
 
Tukio hilo lilitokea mara baada ya meneja Luis Enrique kushindwa kumzawadia pigo la adhabu ndogo mshambuliaji Lionel Messi wakati wa zoezi-mechi iliyokuwa ikichezeshwa na meneja huyo.

Messi alilalama kuwa alikuwa amefanyiwa madhambi na mwalimu hakuonekana kujali, hali hiyo ilisabibisha mzozo mkubwa ulioendelea hadi nje ya uwanja mara baada ya mazoezi kumalizika.

Mara baada ya mhezo huo Messi alikwenda kumlaumu meneja huyo hali iliyopelekea mambo kubadilika na kuwa mabaya zaidi na kupelekea wawili hao kutaka kushikana mashati kabla ya mshambuliaji raia wa Brazil Neymar, kuingilia kati na kuwatenganisha wawili hao huku Messi akiendelea kumrushia maneno meneja huyo.

Post a Comment

 
Top