
Wachezaji hao hawakuandamana na kikosi cha timu hiyo kilicho kilichokwenda kujiandaa kwaajili ya michuano mbalimbali kwenye kambi ya nchini Morocco mara baada ya kuamua kuchelewa ili wapate muda wa kukaa na familia zao.
Ikumbukwe kuwa wawili hao, Cavani na Lavezzi wamekua wakihusishwa na kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo inayotarajiwa kumenyana na klabu ya Montpellier kwenye michuano ya Coupe de France mnamo siku ya kesho jumaatatu.
PSG imewaamuru wawili hao kufanya mazoezi kando na wenzao na ukiachilia mbali mchezo dhidi ya Montpellier lakini pia watakua watazamaji kwenye dimba la
Stade de la Mosson na tripu ya siku ya jumaapili kwenda kupambana na Bastia kwaajili ya mchezo wa Fench League 1.
Post a Comment