0
View image on Twitter
Mustakabali wa mshambuliaji raia wa Colombia Radamel Falcao ndani ya klabu ya Manchester United uko mashakani kufuatia mshambuliaji huyo kuamua kuondoka kwenye viwanja vya Old Trafford mara baada ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha Manchester united kilichotarajiwa kuikabili klabu ya Watakatifu wa Southampton.

Mshambuliaji huyo anayelipwa mshahara wa paundi 346,000 kwa wiki hakutaka hata kuutazama mchezo huo ambao timu yake iliambulia kichapo cha goli 1:0 kwani aliondoka na usafiri wake binafsi kabla hata ya mchezo kuanza.

Falcao storms out of Old Trafford after being axed from United squad

Meneja wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na sababu za kimsingi za kumuacha mshambuliaji huyo alisema kuwa alifanya hivyo ili kuwapa nafasi ya kuwepo kikosini walinzi Jonny Evans, Paddy McNair na Tyler Blackett na mshambuliaji James Wilson.

Falcao, ameanzishwa kwenye michezo takribani saba tu tangu alipotua Ot na kufanikiwa kuwafungia mashetani wekundu hao jumla ya magoli mawili muhimu ambayo yameisaidia klabu hiyo kupata alama muhimu kwenye michezo dhidi ya Stoke na Aston Villa.

Post a Comment

 
Top