
Katika kuhakikisha kuwa meneja wa klbu ya Chelsea anatua ndani ya viwanja vya Wakatalunya pindi tu atakapoutwaa uraisi wa klabu hiyo Joan Laporta amekutana na wakala wa Jose
Mourinho, Jorge Mendes ili kufanya naye mazungumzo ya awali kuhakikisa kuwa dili hilo linakamilika.
Mreno huyo ameibuka kuwa miongoni mwa vipaumbele vya mgombea uraisi huyo wa klabu ya Barcelona Joan Laporta anayepigania nafasi ya kuchaguliwa kuwa raisi wa klabu ya Barcelona kwenye uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mnamo mwaka 2016.
Kwa mujibu wa Redio moja la nchini Hispania ya El Larguero imedai kuwa Laporta amefanya mazungumzo na wakala huyo hapo jana kwenye mmoja wa mikahawa ya nchini Hispania alipomwalika kwenye chakula cha usiku.
Kwa mujibu wa kituo hicho cha redio kimedai kuwa mazungumzo baina ya wawili hao hayakuishia hapo kwani tayari raisi huyo mtarajiwa ametumia nafasi hiyo kuulizia uwezekano wa kumchukua na Cristiano Ronaldo kutoka kwa mahasimu wao wakubwa klabu ya Real Madrid.
Post a Comment