
Kiungo wa klabu ya Mancester United,Ander Herrera ameripotiwa kuwa yuko katika dimbwi zito la kufikiria kuachana na klabu hiyo kwenye dirisha la usajili mnamo mwezi January mara baada ya kushindwa kumuonesha uwezo mzuri meneja wa timu hiyo Louis van Gaal.
Herrera, aliyesajiliwa kutoka kwa klabu ya Athletic Bilbao kwenye majira ya kiangazi alikua na mwanzo mzuri sana mwanzono mwa msimu huu lakini kwa sasa mchezaji huyo kwa sasa anaonekana kuanza kukalia kuti kavu ndani ya Old Traffor.
Taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kuwa kiungo huyo anaweza kuondoka ndani ya klabu hiyo mnamo mwezi january mwakani na tayari inasemekana klabu ya Manchester United iko tayari kumuuza mchezaji huyo kwa ada inayokadiriwa kuwa ni paundi milioni 19.
Post a Comment