0
Avram Grant
Meneja wa zamani wa klabu ya Chelsea Avram Grant ametajwa kuwa ni mtu muafaka na chama cha soka nchini Ghana kuwa huenda ndiye atakayekuwa Meneja mpya wa timu ya Taifa ya Ghana licha ya kuwa dili hilo bado halijakamilika.

Grant, aliyewahi kuvifundisha vilabu vya Portsmouth na West Ham kwa nyakati tofauti kwa sasa ni Mkurugenzi wa ufundi wa moja ya klabu ya nchini Thailand ya Tero Sasana kazi ambayo aliipata mara kachia ngazi ya kazi ya umeneja wa klabu ya Partizan Belgrade mnamo mwezi May 2012.

Grant yuko kwenye orodha ya makocha takribani watano wanaowania nafasi hiyo ya kukinoa kikosi cha  Black Stars wengine wakiwa ni kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Italy Marco Tardelli, Muhispania Juan Ignacio Martínez na Mjerumani Bernd Schuster.

Raisi wa GFA, Kwesi Nyantakyi, amesema licha ya kuwa na orodha hiyo lakini wao kama chama cha soka chaguo lao ni Grant licha ya kuwa atatakiwa kukamilisha mkataba wake wa sasa ili ndio aanze kazi yake hiyo mpya iwapo watakubaliana na chaguo lao la pili liko kwa Muhispania Martinez.
 
 

Post a Comment

 
Top