Michuano ya soka kuwania ubingwa wa bara Afrika kwa wachezaji
wanaocheza soka nyumbani CHAN, inaendelea kupamba moto katika viwanja
mbalimbali nchini Rwanda.
Rwanda
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tayari zimefuzu katika hatua ya
robo fainali baada ya kuandikisha ushindi katika michuano yao miwili
katika kundi A na B.
Kundi A.
Wenyeji Rwanda, wamejumuishwa katika kundi moja na Ivory Coast, Morroco na Gabon.
Amavubi
Stars wanaongoza kwa alama sita baada ya kushinda mchuano wao dhidi ya
Ivory Coast bao 1 kwa 0 na baadaye Gabon mabao 2 kwa 1.
Mchuano unaosalia kutamatisha kundi hili ni dhidi ya Morocco siku ya Jumapili.
Ivory
Coast ambayo ni ya pili katika kundi hili kwa alama tatu, iko katika
nafasi nzuri ya kufuzu ikiwa itaishinda Gabon siku ya Jumapili.
Gabon
pia ina nafasi nzuri ikiwa itashinda mchuano huo na kuomba kuwa Rwanda
inaifunga Morroco au inatoka sare kwa sababu, Morroco nayo ina alama
moja.
Kundi B.
Mabingwa
wa mwaka 2009, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaongoza kundi hili
kwa alama sita baada ya kushinda michuano yake miwili dhidi ya Ethiopia
kwa kuwafunga mabao 3 kwa 0 na kuifunga Angola mabao 4 kwa 2.
Mchuano wake wa mwisho kutamatisha kundi hili ni siku ya Jumatatu dhidi ya Cameroon katika uwanja wa Huye mjini Butare.
Cameroon ni wa pili katika kundi hili kwa alama 4 na mchuano wake na DRC ni muhimu kwa sababu inahitaji ushindi.
Ethiopia
ambayo ina alama moja pia bado ina nafasi ya kusonga mbele ikiwa
itaishinda Angola pia siku ya Jumatatu, ambayo tayari imeondolewa baada
ya kufungwa mechi zake mbili .
Kundi C.
Hadi sasa kundi hili linaongozwa na Nigeria ambayo ina alama 4.
Super
Eagles iliishinda Niger mabao 4 kwa 1 katika mchuano wake wa kwanza
lakini ikatoka sare ya bao 1 kwa 1 na Tunisia siku ya Ijumaa.
Mchuano
wa mwisho wa Nigeria katika kundi hili utakuwa dhidi ya Guinea siku ya
Jumanne juma lijalo katika uwanja wa Umuganda mjini Gisenyi.
Tunisia ambayo ni ya pili kwa alama 2 bado ina nafasi ya kufuzu ikiwa itaishinda Niger juma lijalo.
Niger na Guinea pia wana alama nafasi ya kufuzu.Guinea ina alama mbili huku Niger ikiwa na alama moja.
Siku ya Ijumaa, Guinea na Nigeria zilitoka sare ya mabao 2 kwa 2.
Kundi hili ni gumu kwa sababu hakuna aliye na uhakika wa kufuzu moja kwa moja.
Mshambuliaji wa Nigeria Chisom Chikatara anaongoza katika safu ya ufungaji wa mabao na hadi sasa ameifungia nchi yake mabao 3.
Kundi D
Michuano ya pili ya kundi hili inapigwa siku ya Jumamosi jioni katika uwanja wa Umuganda mjini Gisenyi.
Hadi sasa kundi hili linaoongozwa na Zambia kwa alama 3 ambayo iliishinda Zimbabwe kwa bao 1 kwa 0 mapema juma hili.
Mali na Uganda zina alama 1 baada ya kutoka sare ya mabao 2 kwa 2.
Jumamosi jioni, Zimbabwe wanamenyana na Mali na baadaye Uganda na Zambia.
Michuano ya kundi hili itachezwa siku ya Jumatano, Uganda itamenyana na Zimbabwe na Zambia itamaliza kazi na Mali.
Post a Comment