0
Muda mchache ujao kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es salaam panatarajiwa kuwa na mchezo mkali na wakukata na shoka wa ligi kuu tanzania bara baina ya klabu ya Dar es salaam Young Africans (Yanga)  ya jijini humo dhidi ya Wanalizombe Majimaji ya kutoka Songea Ruvuma.

Kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kutokana na matokeo ya timuzote mbili kwenye michezo yao iliyopita majimaji inaingia kwenye mchezo huo bila ya mshambuliaji wake mkongwe aliyewahi kuzichezea klabu za Simba na Yanga danny Mrwanda ambaye kwa mujibu wa daktari wa timu ya Majimaji Shabani Mbotto anasumbuliwa na majereha kwenye moja ya bega lake.

Majimaji inatarajiwa kuendelea kuzipata huduma za mlinzi wake wa kati aliyewahi kuzitumikia klabu za Moro United na Yanga Lulanga Mapunda almaarufu Anko ambeye amejiunga na timu ya majimaji akitokea klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Lipuli ya mjini Iringa.

Kikosi cha Majimaji kinachotarajiwa kuanza kwenye mchezo wa leo ni;
1. David      Buruhani.
2. Bahati      Yusuphu.
3. Mpoki       Mwakinyuke.
4. Sadick      Gawaza.
5. Lulanga     Mapunda.
6. Alex       Kondo   (C)
7. Peter         Mapunda
8. Paul        Maona
9. Sixmund     Mwasekaga.
10. Frank       Sekule.
11. Marcel      Bonavanture

Kikosi cha Akiba

1. Oddo        Nombo.
2. Peter       Joseph.
3. Kenedy   Kipepe.
4. Hassan     Hamis.
5. Luka      Kikoti.
6. Abubakari     Bakari.
7. Godifrey     Taita

Post a Comment

 
Top