0
Wakati washambuliaji wawili raia wa Uingereza wakiwa ndio habari ya mjini kwenye medani za soka na usajiri nchini humo kumeibuka mjadala kuwa washambuliaji hao Raheem Sterling na Harry Kane wanatajwa kuwa wamebandikwa mabango yanayoonesha kuwa na bei kubwa kupita maelezo.

Mmoja kati ya watu walioonesha masikitiko hayo ni mlinzi wa zamani wa klabu ya Man United Rio Ferdinand ambaye naye anaamini kuwa wachezaji raia wa nchi hiyo wanalipwa na kuuzwa kwa pesa nyingi sana.

Hii inatokana na matakwa ya pesa nyingi ya klabu ya Liverpool kwaajili ya mauzo ya Raheem Sterling na mshambuliaji wa Tottenham  Harry Kane.

Sterling anafukuziwa na klabu ya Manchester City, wakati mwingereza mwenziwe Kane aliyefunga jumla ya magoli 31 kwenye mashindano yote msimu uliokwisha akiwa na Spurs ametajwa kuwaniwa na klabu ya Manchester United.

Ferdinand, aliyestaafu soka mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita akiwa na klabu ya QPR, alishawahi kugonga vichwa kwenye vyombo vya habari ulimwenguni mnamo mwaka 2002 alipohama kutoka klabu ya Leeds United kwenda Manchester United kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 18.

Akitoa maoni yake kuhusiana na masuala mbalimbali ya usajili yanavyoendelea nchini Uingereza mlinzi huyo wa kati wa zamani wa klabu ya West Ham alisema anaamini kuwa wachzaji wa kiingereza wanalipwa fedha nyingi sana kwaajili ya uhamisho kuliko uwezo wao na akafananisha ada za uhamisho za wachezaji kama washambuliaji wa vilabu vya Manchester City,  Sergio Aguero na  Alexis Sanchez wa Arsenal.

"Wachezaji wa Uingereza wanalipwa pesa nyingi sana siku hizi, haya ni masihara jamani,"
"Kane na Sterling ni wachezaji wenye uwezo mkubwa sana lakini paundi milioni 40 kwa Kane na 50 kwa Sterling sio sawa kabisa wakati Aguero alilipiwa kiasi cha paundi milioni 38 na Sanchez 32" Ameandika Ferdinand kwenye ukurasa wake rasmi wa tweeter.

Post a Comment

 
Top