0
Abasalim Chidiebele atua Coastal Union

HATIMAYE timu ya Coastal Union imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Stand United Mnigeria Abasalim Chidiebele kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Chidiebele aliyeshika nafasi ya tatu kwa ufungaji kwenye ligi ya msimu uliopita amethibitisha hilo kwa kusema ametua Coastal Union baada ya kuvutiwa kwa ofa ambayo wamempa na kuahidi atahakikisha anajituma ili azidi kufanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa Stand.

Meneja wa Coastal Union, Akida Machai amesema kwa muda mrefu walikuwa wakimfuatilia mshambuliaji huyo na baada ya kumnasa sasa wanauhakika watafanya vizuri msimu ujao na kubigania ubingwa wa Tanzania bara.

Coastal Union ipo katika harakati za kukijenga upya kikosi chake baada ya kuvunja mikataba ya idadi kubwa ya wachezaji wake iliyokuwa nao msimu uliopita kwa matatizo mbalimbali.

Post a Comment

 
Top