0
Aliyekuwa kocha waklabu ya Chelsea Jose Mourinho.

Kocha aliyefungashiwa virago na klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema anataka athibitishiwe na mabosi wa klabu ya Manchester United kama atakua meneja ajaye wa klabu hiyo gazeti la The Sun la nchini Uingereza limeandika.

Kocha huyo mwenye maneno mengi amekua akihusushwa kujiunga na Mashetani wekundu wa jiji la Manchester lakini kura ya kua na imani na mwalimu wa sasa wa timu hiyo Luis van Gaal kutoka kwa aliyekua kocha wa timu hiyo Sir Alex Furguson inaongeza uwezekano wa kocha huyo kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Kocha huyo sasa anataka ahakikishiwe ajira hiyo mapema ili kama nafasi hiyo itaendelea kutumikiwa na kocha huyo basi yeye aangalie utaratibu mwingine kwa kutafuta ajira mahala pengine.

Post a Comment

 
Top