
KOCHA Hans van der Pluijm, leo Jumapili ataingia
majaribuni ya kutetea ubingwa wake wa Ligi ya Vodacom Tanzania bara
wakati itakapokuwa nyumbani uwanja wa taifa Dar es Salaam kuwaalika
Coastal Union ya Tanga.
Huo utakuwa ni mchezo pekee kwa siku ya leo ikiwa ni siku ya pili tangu
kuanza kwa msimu mpya wa Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri mbele ya
Coastal Union,ambayo msimu uliopita iliweza kushinda mechi zote mbili
ikiwemo kupata ushindi mnono wa mabao 8-0 katika mchezo wa marudiano
uliofanyika uwanja huo wa taifa.
Kinachompa matumaini ya kushinda mchezo huo kocha Pluijm, wa Yanga ni
usajili walioufanya kwa kuongeza wachezaji wapya saba kwenye kikosi
chake wakiwemo nyota wakimataia Donald Ngoma na Thaban Kamusoko wa
Zambabwe na wazawa Malimi Busungu,Mateo Simon ,Haji Mwinyi na Vicent
Bossou raia wa Togo.
Kuwepo kwa nyota hao kunaonekana kukiimarisha zaidi kikosi cha Yanga
ambacho katika mchezo wa leo kitawakosa mrisho Ngassa na Kpah Sherman
ambao wamesajiliwa na timu za Afrika Kusini.
Katika mchezo wa leo niwazi Pluijm, atataka kuanza kwa kutoa onyo
kwa kupata ushindi mnono ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuongoza
ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa msimu huu.
Wachezaji kama Ngoma,Kamusoko wanatarajia kuanza kikosi cha kwanza
huku kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ akianzia golini huku akilindwa na
mabeki Nadir Haroub na Kelvini Yondani.
Beki wa kushoto Haji Mwinyi, anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi cha
Pluijm, kwa ajili ya kusaidia mashambulizi ya upande wa kushoto kwa
kupiga krosi ambazo zitakuwa zikiwakuta akina Ngoma na Amissi Tambwe,
ambao kazi yao kubwa itakuwa ni kihakikisha nyavu zinacheza.
Pluijm amesema, aahitaji kupata ushindi wa mabao 3 kwenda
mbele kutokana na uimara wa kikosi chake na ukali wa safu yake ya
ushambuliaji.
“Nimchezo mwepesi ambao hauniumizi kichwa kama kocha kwasababu ya
ubora wa kikosi changu na mapungufu waliyokuwa nayo wapinzani wetu
Coastal Union,”amesema Pluijm.
Kwaupande wake kocha wa Coastal Union Jackson Mayanja, ametamba kuwa
wapo Dar es Salaam kuhakikisha wanapata ushindi na hawaihofii Yanga
kwasababu kwake ni timu kama zilivyo timu nyingine.
Mayanja mabaye msimu uliopita alikuwa akiifundisha Kagera Sugar
amesema anazijua vyema mbinu za kocha Pluijm, wa Yanga na mara zote
amekuwa akiifunga Yanga wakati akifundisha Kagera.
“Tunacheza na Yanga nikweli timu kubwa na tunawaheshimu kwakua ni
mabingwa lakini tumejipanga kuwafunga wakiwa nyumbani,”amesema Mayanja.
Mayanja kwa kiasi kikubwa amekibadilisha kikosi cha Coastal kwa
kusajili sura nyingi mpya akiwemo Chidiabele Abasalim raia wa Nigeria
ambaye alishika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji msimu
uliopita.
Pia kwenye kikosi hicho yupo Twaha Shekuhe ‘Messi’ aliyekuwa
akiichezea Simba mchanganyiko huo ndiyo unaotarajiwa kusababisha
ushindani mkali kwenye mchezo huo wa leo.
Chanzo; Goal.com
Post a Comment